Friday 24 February 2017

MWENDELEZO WA KIKAO CHA BARAZA MAPEMA HII LEO TAREHE 24/02/2017

Katika kuboresha ukuaji wa Wakala na wafanyakazi wake kwa ujumla Baraza la wafanyakazi limekutana tena hii leo ili kujadili mstakabadhi huo ambao utaleta manufaa kwa Wakala, wafanyakazi na Taifa kwa ujumla. (habari katika picha)




Thursday 23 February 2017

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI CHAFANYIKA NHBRA

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi NHBRA wamekutana ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu utendaji wenye tija katika kuimarisha ukuaji wa Wakala pamoja na wafanyakazi wake.

Katibu wa Baraza la Wafanyakazi NHBRA Mhandisi Twwimanye John akimkaribisha Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt. Matiko S. Mturi (wa kwanza kulia) ili amkaribishe mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa Baraza, Dkt Mturi (aliyesimama) akimkaribisha Mgeni Rasmi kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa kikao hicho
Mgeni rasmi, Mhandisi Amani Msuya akihutubia wajumbe wa Baraza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho

 

Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi mapema leo tarehe 23/02/2017 NHBRA-Dar es Salaam

Tuesday 7 February 2017

UNUNUZI WA VIFAA VYA UJENZI VIPATIKANAVYO NHBRA

Wateja wengi wamekuwa wakijiuliza namna ya kupata na kununua vifaa vyetu vya ujenzi hasahasa kama wako mikoani.
Jibu la swali hilo ni:

Unatakiwa uingize hela ya mashine na ya usafiri kwa eneo ulipo kwenye akaunti ya NHBRA ambayo ni A/C No. 20101100130 National Micro Finance Bank (NMB) na kutuma risiti ya benki NHBRA ikiwa na anuani yako kamili. Baada ya hapo utatumiwa mashine yako.

Pia kwa wateja wetu waishio maeneo ya karibu mfano Dar es Salaam malipo yote yana paswa kupelekwa benki na kuleta tuu risiti ya benki katika ofisi zetu.

Zifutazo ni gharama za Vifaa vya Ujenzi:
Mashine ya kufyatulia matofali ya kufungamana ni sh 650,000/-
Mashine ya Vigae mkonge ni sh 250,000/-
Kalibu za vigae (moulds) ni sh 25,000/-@

Kwa taarifa Zaidi tembelea tovuti yetu
http://www.nhbra.go.tz/howdo/5

Au piga simu
+255 679 972 715