Friday, 28 August 2015

NHBRA YATEMBELEWA NA UGENI KUTOKA JAMHURI YA CHINA

Wageni kutoka China wakiongozwa na Mr Han Jinsheng (wa nne kutoka kulia mstari wa mbele) The Vice Director, Shanxi Provincial Geological Prospection Bureau pamoja na timu yake walipotembelea NHBRA siku ya tarehe 25 Agosti, 2015.

Wageni kutoka China wakiwa katika pichaya pamoja na menejimenti ya NHBRA na baadhi ya Wakurugenzi wa idara mbalimbali kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

 
Wageni wakiangalia namna ya kutengeneza vigae vya mkonge vya kuezekea nyumba.

 
Fundi Sanifu Hussein Mataka akionesha tofali la kufungamana alilolifyatua wakati akionyesha namna ya kutengeneza matofali hayo kwa wageni hao.
 
Mgeni akichukua tofali hilo ili kuliangalia vizuri baada ya kufyatuliwa.
 
Wageni wakiangalia tofali la kufungamana baada ya kufyatuliwa.

Wageni wakilishangaa tofali la kufungamana lililofyatuliwa kwa ajili yao huku wakishuhudiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu (wa pili kushoto) na Mhandisi Mwandamizi, Amri Juma (wa kwanza kushoto).
 Tuesday, 4 August 2015

Usikubali kuhadithiwa, njoo katika banda la NHBRA ujionee vifaa vya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, ni wakati wako sasa Mwananchi wa Lindi na maeneo ya jirani, tumia fursa hii, tukutane Ngongo husani banda la NHBRA. Usikose!
Monday, 3 August 2015

Wananchi wa Kanda ya Kusini, Mikoa ya Lindi na Mtwara ni fursa yenu kutembelea banda la NHBRA katika maonesho ya Nane Nane lililopo huko Ngongo Lindi. Tumia nafasi hii uweze kupata elimu na fursa ya kujua zaidi kuhusu teknolojia ya ujenzi wa gharama nafuu kwa kutumia matofali ya kufungamana pamoja na vigae mkonge, mwananchi usijishauri, njoo ujionee mwenyewe na upate elimu hii adhimu ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, nyote mnakaribishwa.

Saturday, 1 August 2015

Tembelea banda la NHBRA upate kujua mengi kuhusu vifaa vya ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu, karibuni sana!!

Karibuni katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa Mkoani Lindi eneo la Ngongo. Msikose kutembelea banda la NHBRA ili kujionea vifaa vya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Wote mnakaribishwa