Tuesday, 18 September 2018

KAIMU MKURUGENZI WA NHBRA ATEMBELEA KARAKANA NA WAKALA

Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Bw. Dismass Minja, alipata nafasi ya kuangalia baadhi ya Tafiti zilizofanywa na Wakala pamoja na Tafiti nyingine zinazoendelea.

Meneja wa Utafiti Eng. Benedict Chilla akitoa maelezo ya Tafiti zinazoendelea juu vigae vya kuchoma, kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wakala Bw. Dismass Minja 


Kaimu Mkurugenzi wa NHBRA akiangalia utengenezaji wa ''Waffles'' ambayo pia ni miongoni mwa Tafiti zilizokamilika. Teknolojia hii mpya kwa Tanzania hutumika zaidi katika ujengaji wa nyumba za ghorofa 

Fundi Sanifu akitoa maelezo juu ya mashine ya kufyatulia matofali ya kufungamana ambayo bado iko kwenye tafiti yenye uwezo wa kutoa matofali mawili.

Meneja Utafiti na Maendeleo akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi juu ya utengenezaji wa kigae mkonge
Kaimu Mkurugenzi akiangalia fremu ya mlango wa zege ambayo tayari imeshawekwa ukutani. Fremu hizo zimeonekana kuwa zitakuwa suluhisho kubwa kwa Watanzania wanaolalamika mchwa kuharibu milango yao
Kaimu Mkurugenzi akiangalia ufyatuaji wa tofali la kufungamana


Kaimu Mkurugenzi akifanya jaribio la kutoa tofali katika mashine ya kufungamana

Kwa mawasiliano zaidi juu ya namna ya kupata mashine ya matofali ya kufungamana, kununua tofali, vigae mkonge na kupata mafunzo usisite kututafuta kwa namba ifuatayo;

0679972715

au

Barua pepe: dawatilamsaada@nhbra.go.tz

au

Fika ofisini kwetu Mwenge tunapakana na kituo cha mafuta cha Oilcom.

Karibuni sana.

Monday, 3 September 2018

JESHI LA MAGEREZA LAVUTIWA NA TEKNOLOJIA YA UJENZI WA GHARAMA NAFUU

Jeshi la Magereza (Tanzania Prison Service) haliko nyuma katika kusambaza teknolojia ya ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu. Baadhi ya Askari wa Jeshi hilo kutoka Lindi na Tanga walifika NHBRA kuanzia tarehe 20/08/2018-02/09/2018 kwa ajili ya kupata mafunzo ya namna ya kutumia mashine ya matofali ya kufungamana na jinsi ya kujenga kwa kutumia tofali hizo ambapo pia waliahidi kusambaza teknolojia hii kwa jamii iliyowazunguka. 

Askari kutoka Jeshi la Magereza wakiwa kwenye jaribio la kufyatua tofali la kufungamana katika ofisi za NHBRA


Washiriki kutoka Jeshi la Magereza wakitoa tofali la kufungamana kutoka kwenye mashine ya matofali ya kufungamana

Askari wa Jeshi la Magereza wakifanya setting ya nyumba katika mafunzo ya ujenzi wa nyumba kwa kutumia matofali ya kufungamana yanayotolewa na NHBRAIli kuweza kupata mafunzo kama haya, mteja unashauriwa kununua mashine ya matofali ya kufungamana kwa gharama ya shilingi 650,000/- ambapo malipo hayo mteja atapaswa kulipia benki. Na baada ya kununua mashine Mteja atapata mafunzo kwa vitendo juu ya utumiaji wa mashine ya tofali za kufungamana pamoja na namna ya kujenga kwa muda wa wiki moja kulingana na uelewa wa vijana ambao Mteja atakuwa amewaleta wasiozidi watatu.

Kwa mawasiliano zaidi, usisite kututafuta kwa namba ifuatayo;

0679972715

au

Barua pepe: dawatilamsaada@nhbra.go.tz

au

Fika ofisini kwetu Mwenge tunapakana na kituo cha mafuta cha Oilcom.

Karibuni sana.