Monday, 16 April 2018

USAMBAZAJI WA TEKNOLOJIA YA UJENZI WA GHARAMA NAFUU

Moja wapo ya jukumu la Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi ni kusambaza matokeo ya tafiti zake kwa njia mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo kwa vikundi au mtu mmoja mmoja.

Pichani ni baadhi ya vikundi vilivyotutembelea katika ofisi zetu Mwenge, Dar es Salaam kwa ajili ya kupata mafunzo juu ya ujenzi wa gharama nafuu kwa kutumia matofali ya kufungamana pamoja na vigae mkonge.
Kwa mawasiliano zaidi juu ya namna ya kupata mafunzo na kununua mashine za matofali ya kufungamana au vigae mkonge, usisite kututafuta;

Barua pepe: dawatilamsaada@nhbra.go.tz

Namba ya Simu: +255 679 972 715


Thursday, 8 March 2018

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

NHBRA hatukuwa nyuma katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika jana  tarehe 8/03/2018 katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Kauli mbio ya maadhimisho hayo ni ''kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake vijijini na mijini''.

HABARI PICHATuesday, 6 March 2018

VIJUE VIGAE MKONGE

Vigae Mkonge ni aina mojawapo ya vigae vitumikavyo katika kuezekea nyumba. Katika utengenezaji wa vigae hivyo zifuatazo ni orodha ya vitu vinavyowekwa katika mchanganyo ili kuweza kupata kigae mkonge:

 • Saruji
 • Mchanga
 • Nyuzi za katani zitokanazo na zao la mkonge ambazo hutumika ili kuongeza uimara wa kigae
 • Rangi

Kutokakana na utafiti uliofanywa na NHBRA imeonekana kuwa vigae mkonge ni mkombozi kwa
wananchi wa kawaida hasa wa kipato cha wastani na cha chini kwa kuwa utengenezaji wake hutokana na vifaa vipatikanavyo hapa nchini na huweza kutengenezwa na mtu mmoja mmoja, ama vikundi mahali popote mijini na vijijini ili kuboresha makazi.

Utengenezaji wa Vigae Mkonge

Utengenezaji wa vigae mkonge ni lazima uwe na vifaa vifuatavyo: 

 • Mashine mtetemo (Vibrating Machine)
 • Saruji
 • Mchanga
 • Nyuzi za katani
 • Rangi
 • Maji safi
 • Pasi mwashi
 • Mwiko mwashi
 • Kizoleo
 • Chepe

Kigae mkonge kikiwa katika mashine mtetemo

kigae mkonge kikiwa kimewekwa kwenye kalibu ili kutengeneza umbo la kigae hicho

Kwa maswali au maoni usisite kututafuta
Barua pepe

dawatilamsaada@nhbra.go.tz

Tuesday, 20 February 2018

MAFUNZO YAKIENDELEA

Pichani ni wanachama wa Asasi isiyo ya kiserikali ''Hyperactive Solution Center'' wakiendelea kupata mafunzo ya namna ya kutengeneza vigae mkonge katika ofisi za NHBRA, Dar es Salaam.
Monday, 19 February 2018

MAFUNZO KWA VITENDO

Moja wapo ya kazi zinazofanywa na Wakala ni kusambaza ujuzi wa ujenzi kwa kutumia vifaa vya gharama nafuu. 

Pichani ni wanachama wa asasi isiyo ya kiserikali ''Hyperactive Solution Center'' wakifanya zoezi la kufyatua tofali kwa kutumia mashine ya matofali ya kufungamana ''Interlocking bricks press machine'' katika ofisi za NHBRA zilizopo Mwenge, Dar es Salaam.
Kwa mawasiliano zaidi juu ya namna ya kupata mafunzo au kununua bidhaa zetu usisite kututafuta kwa namba zifuatazo

+255 679 972 715

au

barua pepe: dawatilamsaada@nhbra.go.tz

Monday, 11 December 2017

SHULE ZA SEKONDARI TABORA ''BOYS'' NA TABORA ''GIRLS'' ZANEEMEKA

Katika maboresho yanayofanyika kwenye shule kongwe za Serikali NHBRA ilipata nafasi ya kusimamia ukarabati wa majengo ya Shule za Tabora ''boys'' pamoja na Tabora ''girls''. Zifuatazo ni baadhi ya picha zikionyesha maeneo yaliyofanyiwa ukarabati huo;

Maabara ya Kemia iliyofanyiwa ukarabati na NHBRA katika Shule ya Sekondari Tabora ''girls''

Muonekano wa ndani wa jengo jipya la maktaba ya kisasa lililojengwa na NHBRA katika Shule ya Sekondari Tabora ''boys''

Muonekano wa nje wa maktaba iliyojengwa na NHBRA Shuleni Tabora ''boys''

Sunday, 10 December 2017

VIGAE VIPATIKANAVYO NHBRA


Utengenezaji wa kigae cha mkonge ukiendelea kwa kutumia mashine mtetemo ipatikanayo NHBRA

Kigae mkonge kikiwa kwenye kalibu kwa ajili ya kupata umbo na baada ya masaa 24 kuingizwa kwenye maji kwa ajili ya kukikomaza

Vigae vikiwa tayari kwa matumizi
Kwa mawasiliano zaidi, usisite kututafuta kwa namba ifuatayo;

0679972715
au

Barua pepe: dawatilamsaada@nhbra.go.tz
au

Fika ofisini kwetu Mwenge tunapakana na kituo cha mafuta cha Oilcom