Monday, 30 July 2018

WAFANYAKAZI WA NHBRA WAONGEZEWA UWEZO

NHBRA ilipata nafasi ya kuhudhuria semina ya Uhamasishaji kwa watumishi ili kusaidia katika kuongeza ufanisi katika majukumu ya kila siku wawapo kazini. Mada mbalimbali zilitolewa mfano namna ya Utendaji kazi Serikalini, maadili katika Utumishi wa Umma n.k. Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa UDBS-UDSM.
Semina hiyo ilihudhuriwa na watoa mada kutoka Utumishi ya Umma pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

HABARI PICHA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHBRA akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye semina ya uhamasishaji kwa watumishi wa Wakala kwenye ukumbi wa UDBS-UDSM


Kaimu Meneja wa Biashara na Utawala wa NHBRA Bi. Hadija Maloya akitoa ufafanuzi juu ya huduma zitolewazo katika kitengo cha Biashara
Tuesday, 3 July 2018

TUPO SABASABA

Tunautangazia Umma kwamba Nhbra Tanzania inashiriki Maonyesho ya 42 ya Kitaifa ya Biashara-Sabasaba. Tembelea Banda letu lililopo katika hema la Katavi Banda namba 11-13 ili upate kufahamu na kujionea tafiti zetu kama mashine za matofali ya kufungamana, nyumba ndogo ya mfano iliyojengwa kwa tofali za kufungamana na kuezekwa kwa kutumia vigae vya gharama nafuu, pamoja na teknolojia yetu mpya ya fremu za milango za zege pamoja na sakafu ya dari "waffles"... KARIBUNI SANAAAAAAA tuko hapa mpaka tarehe 13/7/2018.

Moja wapo ya teknolojia mpya za ujenzi tulizoenda nazo sabasaba ni ujenzi kwa kutumia ''waffles'' kama ilivyo kwenye picha upande wa kushoto ni mwonekano wa waffles ikiwa tayari imejengwa kwa mfano wa ujenzi wa nyumba ya ghorofa. karibuni sabasaba mje mpate maelezo ya kina juu ya teknolojia hii.

Mwonekano wa banda letu sabasaba

Baadhi ya washiriki kutoka NHBRA wakiwa tayari kutoa maelezo ya kina kuhusu teknolojia ya gharama nafuu

Mgeni aliyetutembelea akipata maelezo kuhusu teknolojia yetu mpya ya kujenga nyumba ya ghorofa kwa kutumia ''waffles''

Mgeni alietutembelea akiangalia kwa umakini teknolojia yetu mpya ya ujenzi wa nyumba ya ghorofa kwa kutumia waffles


Wananchi wakipata maelezo juu ya utengenezaji wa tofali za kufungamana
Karibuni sanaaaaa......