Friday 11 May 2018

HATUA ZA UTENGENEZAJI WA VIGAE MKONGE

Mojawapo ya tafiti za NHBRA ni utengenezaji wa Kigae mkonge, ambacho mpaka sasa tumefanikiwa kupata wateja wengi ambao wamenunua vigae kwa ajili ya kupaulia nyumba zao.
Vile vile ni fursa kwa ajili ya Watanzania kufanya ujasiriamali kwa kupitia utengenezaji huu wa kigae mkonge. Wateja wengi ikiwamo vikundi mbalimbali kama Taasisi zisizo za Serikali, wamefika ofisini kwetu na kununua mashine ya kutengeneza vigae mkonge na walipatiwa mafunzo ya kina ya namna ya kutengeneza vigae hivyo. 

Wanakikundi cha Hyperactive Solution Center wakipatiwa mafunzo ya namna ya kutengeneza kigae mkonge

Zifuatazo ni hatua katika utengenezaji wa Vigae Mkonge:
  • Changanya saruji na mchanga
  • Weka rangi (optional)
  • Weka nyuzi za mkonge kwa kiasi kinachohitajika
  • Ongeza maji katika mchanganyiko mkavu
  • Weka karatasi ya nailoni juu ya mashine na kukandamiza na fremu ya chuma
  • Jaza mchanganyiko ndani ya fremu ya chuma


  • Tetemesha mchanganyiko ulioko ndani ya fremu
  • Ondoa karatasi lenye mchanganyiko na kuweka juu ya kalibu iliyoandaliwa


  • Acha kigae juu ya kalibu si chini ya saa 12 baada ya hapo vigae lazima vizamishwe kwenye maji si chini ya siku 21 kwa ajili ya kuvikomaza.

Vigae mkonge vikiwa tayari vimekomaa baada ya kutolewa kwenye kisima cha maji
Mfano wa nyumba zilizoezekwa wa kigae mkonge

Mikocheni-Dar es Salaam


Faida za Vigae Mkonge
  • Vifaa vitumikavyo kutengenezea vigae hupatikana nchini
  • Utengenezaji ni rahisi hata kwa mtu asiyekuwa fundi
  • Hupendezesha jengo na kulifanya kuwa na thamani ya juu kwa gharama nafuu
  • Hupozesha joto/baridi na kelele za mvua
  • Vina uzito mdogo
  • Gharama nafuu
  • Hudumu kwa muda mrefu


Kwa mawasiliano zaidi, usisite kututafuta kwa namba ifuatayo;

0679972715

au

Barua pepe: dawatilamsaada@nhbra.go.tz



au

Fika ofisini kwetu Mwenge tunapakana na kituo cha mafuta cha Oilcom



No comments:

Post a Comment