Tuesday, 4 October 2016

SIKU YA MAKAZI DUNIANI

Siku ya Makazi Duniani huadhimishwa Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba kila Mwaka ambapo kwa mwaka 2016 maadhimsho hayo yalifanyika tarehe 3/10/2016 kwenye viwanja vya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu "Nyumba Kitovu cha Miji" yaliongozwa na Mhe. William Lukuvi ambaye ni Waziri wa Wizara hiyo. Katika maadhimisho hayo Wakala wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi ulipata nafasi ya kushiriki maadhimisho hayo kama mdau wa usambazaji wa teknnolojia ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa kutumia tafiti mbalimbali ili kumnufaisha Mtanzania.
Arch. Godfrey Munyaga wa pili kulia akifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kwenye maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani 
Mhe. William Lukuvi akiangalia bango linaloonyesha baadhi ya kazi zilizokwisha fanywa na Wakala wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi, wengine ni Afisa Masoko wa Wakala Bi. Zubeda Salum pamoja na mwakilishi wa Shirika la Nyumba (NHC) 
Mhe. William Lukuvi akipata ufafanuzi juu ya shughuli za Wakala kutoka kwa Bw. Frimin Lyakurwa ambaye ni Msaidizi Mwandamizi wa Maktaba.

No comments:

Post a comment