Ujenzi wa nyumba kwa
kutumia matofali ya kufungamana ni mojawapo ya aina ya ujenzi wa gharama nafuu
ambao huondoa matumizi ya udongo mwashi kama kiunganishi kati ya tofali na
tofali ingawa mambo yote ya msingi na kanuni za ujenzi lazima
vizingatiwe.
Kabla
ya kuanza ujenzi ni lazima kuwe na msingi imara uliojengwa kwa vifaa imara
ambao upo kwenye vipimo sahihi, ili kuweza kutumia tofali hizi. Sehemu ya msingi wa nyumba (substructure) itakuwa na-:
•
Kitako cha
msingi: zege/mawe
•
Ukuta wa
msingi: Matofali ya saruji na mchanga, udongo na saruji yanayofungamana, mawe au
matofali ya kuchoma.
Endapo tofali za
udongo-saruji za kufungamana zitatumika ni lazima unene wa ukuta wa msingi usipungue
sm 30 (urefu wa tofali). Ili kukabiliana na hali ya unyevunyevu ni vyema
kuimarisha zaidi tofali kwa kuongeza kiwango cha saruji kwenye udongo wakati wa
ufyatuaji.
Ujenzi
kwa kutumia matofali ya udongo au udongo ulioimarishwa umeonekana kuwa wa
gharama nafuu zaidi kutokana na upatikanaji wa udongo katika sehemu kubwa nchini.
Katika ujenzi huu tofali
linalotumika huwa na vipimo vifuatvyo:
•
Urefu 300mm
•
Upana 150mm
•
Unene 100mm
Vilevile kuna vipande
vya nusu na robo tatu tofali.
 |
Tofali Zima |
 |
Robotatu tofali |
 |
Nusu tofali |
 |
Tofali Zima |
 |
Robotatu tofali mbili |
 |
Tofali la chaneli |
Kabla ya kuanza
ujenzi ni lazima kupitia ramani iliyopo ili kuona kama inakubaliana na vipimo
vya urefu wa ukuta ambapo ni lazima vigawanyike kwa tofali zima au nusu (yaani 300 au 150mm).
Mfano ukuta wenye
urefu wa mita 3, hujengwa kwa tofali nzima 10, katika mstari mmoja wenye urefu
huo. Ikumbukwe kuwa katika ujenzi huu hatukati vipande vyenye urefu mbalimbali
kama ambavyo hufanyika katika ujenzi wa matofali yasiyofungamana, badala yake
vipande vya nusu na robo tatu hutumika.
Nyumba imegawanyika katika sehemu kuu mbili:-
•
Msingi: Sehemu ya chini ya nyumba (substructure)
•
Boma: sehemu ya juu ya msingi
Msingi: Msingi wa nyumba hujengwa kwa:
•
zege,
•
mawe
•
matofali ya saruji na
mchanga
•
matofali ya udongo na
saruji.
 |
Namna ya kuset matofali ya kufungamana kwenye msingi uliojengwa kwa matofali ya saruji na mchanga. |
Kwa kuwa msingi ndio sehemu inayobeba mzigo wa jengo
zima ni muhimu vifaa vinavyotumika kuujenga viwe bora na imara. Kwa maeneo
yaliyo mengi nchini zege, mawe na tofali za saruji mchanga ndio hutumika
kujenga msingi wa nyumba. Hata hivyo matumizi ya udongo na saruji hutumika kujenga misingi kwa maeneo
yenye udongo imara. Lakini mchanganyiko wake ni lazima uboreshwe zaidi ili
kupata tofali imara lenye uwezo wa kubeba uzito na kuhimili hali ya unyevunyevu.
Boma: Sehemu
hii ya nyumba hujengwa kwa kutumia zege, mawe, matofali ya mchanga na saruji,
matofali ya udongo na saruji, matofali ya udongo na chokaa au matofali ya
udongo. Ujenzi kwa kutumia matofali ya udongo au udongo ulioimarishwa
umeonekana kuwa wa gharama nafuu zaidi ukilingnisha na ujenzi wa matofali ya
saruji na mchanga. (itaendelea toleo lijalo)
 |
Boma lililojengwa kwa kutumia matofali ya kufungmana |
Usikose mwendelezo wa mfunzo haya, tukutane toleo lijalo.......