Friday 17 July 2015

UTENGENEZAJI WA MATOFALI YANAYOFUNGAMANA YA UDONGO SARUJI

Matofali haya yanatumia udongo na saruji katika utengenezaji wake ndio maana yanaitwa matofali ya udongo saruji. udongo wa aina zote unaweza kutumika kutengeneza matofali haya, lakini udongo unaofaa zaidi ni ule wenye kiasi cha mfinyanzi kati ya 10% hadi 40%. Udongo ukiwa na kiasi cha mfinyanzi chini ya 10% udongo huo haufai kutengeneza matofali haya kwani mnato unakuwa mdogo hivyo tofali halitashikamana, kutokana na aina ya mashine zinazotumika  tofali halitaweza kubebeka kutoka katika mashine kwa kuwa mashine inayotumika kutengeneza haitumii vibao kwa ajili ya kubebea. Kiasi cha mfinyanzi kikizidi 40% udongo huo unafaa kuchanganywa na saruji ila hushauriwi kufanya hivyo kwa sababu kiasi cha saruji kinachotumika ni kikubwa hivyo kukuongezea gharama za utengenezaji wa matofali hayo, tofali litanywea baada ya kukauka, hivyo kupasuka kwa sababu ya mfinyanzi kuwa mwingi, pia udongo huo hauwezi kuchanganyika vizuri na saruji kwa kutumia chepe kwa sababu ya mnato mkali au udongo wenye kiasi cha mfinyanzi zaidi ya asilimia arobaini unaweza kupiga matofali bila ya kuchanganya na saruji ila italazimika kuyachoma matofali hayo ili yawe imara zaidi.

 
Ili kujua kiasi cha mfinyanzi kilichopo katika udongo ili kujua kiasi cha saruji kinachohitajika katika kuchanganya na udongo wakati wa kutengeneza matofali yanayofungamana kuna majaribio yanayofanyika ili kuweza kujua hayo yote. majaribio hayo ni:
  1. jaribio la chupa (bottle test)
  2. jaribio la kasha (shrinkage box test)
JARIBIO LA CHUPA

Jaribio hili hutumika kupima kiasi cha mfinyanzi kilichopo katika udongo unaotaka kuutumia,Udongo unaotumika ni udongo wa chini udongo wa juu ni lazima uondolewe kwani ni udongo wenye mbolea na mizizi haufai kwa shughuli za ujenzi, udongo unaofaa ni ule wa chini hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa udongo wote wenye mizizi na mbolea uneondolewa.


 
Picha za jaribio la chupa katika kutambua kiasi cha mfinyanzi katika udongo

 

JARIBIO LA KASHA

Jaribio hili hufanyika ili kujua uwiano wa kuchanganya udongo na saruji ili kuweza kutengeneza matofali yenye ubora unaotakiwa. Kasha linalotumika katika jaribio hili ni kam linavyoonekana katika picha hapo chini.
 
Jaribio likiwa limekamilika, matokeo yanapimwa
 
 
  • Baaada ya kupata majibu katika majaribio  na kupata uwiano wa kuchanganya saruji na udongo hatua za upimaji na uchanganyaji huanza.
  • Udongo uwe mkavu kabisa na kama una chembechembe kubwa udongo unaotumika lazima uchekechwe.
  • Tumia ndoo au karai kupima udongo.
  • Changanya udongo na saruji hadi vichanganyike vizuri
  • Nyunyizia maji hadi udongo uwe na uwezo wa kushikamana lakini usilowe hadi kutengeneza tope.
 
Udongo ukichanganywa na saruji tayari kwa kufyatua matofali.
Mashine ya kutengenezea matofali ni lazima ifungwe kwenye kitako cha mbao kwa kutumia bolt na
nut ili ikae itulie isisumbue wakati wa kufanya kazi ya ufyatuaji matofali pia ni lazima kuiwekea
vilainishi ili kupunguza msuguano wa vyuma wakati wa kufyatua matofali.
 


Hatua za ufyatuaji matofali
 
  • Funua mfuniko wa mashine
  • Jaza udongo kwenye kasha la mashine
  • Funika mfuniko
  • Shindilia
  • Funuo mfuniko
  • Kandamiza ili kutoa tofali kwenye mashine
  • Tofali hubebwa na mtu mmoja kwa mikono miwili na kulipeleka kuweka sehemu iliyoandaliwa
 
Umwagiliaji maji hufanyika kwa muda wa siku saba hadi ishirini na nane tangu yanapofyatuliwa

 
Matofali yakishakauka yanakuwa tayari kutumika katika ujenzi kama picha chini inavyoonyesha.




Jiwezeshe tukuwezeshe, kwa maelezo na huduma wasiliana nasi kwa simu namba +255 22 2771971 au info@nhbra.go.tz

16 comments:

  1. je,mashine hizi zinauzwa bei gani?
    na naweza kuzipataje kwa mkaazi wa tanga kama mimi?

    ReplyDelete
  2. Habari za kazi. Nimekuwa nikiwafuatilia makala zenu na kuuliza maswali mbalimbali lakini hamjibu. Hii haileti picha nzuri kwa wateja.

    ReplyDelete
  3. Mfuko mmoja wa saruji ni ndoo ngapi za udongo

    ReplyDelete
  4. Nahitaji mashine yakufyatua matofari

    ReplyDelete
  5. ninaomba kupata bei ya hiyo machine

    email yangu n; Will250son@gmail.com

    Wilson

    ReplyDelete
  6. Nilikua Nina shida na mashine zenu, za matofali haya, niojua nataka kujia gharama ya mashine inayo fyatua tofali moja moja

    ReplyDelete
  7. +255718466609 namba zangu za ofisi za Whatup jilkua Naomba ishirikiano kujua bei

    ReplyDelete
  8. Nimefurahishwa sana na maelezo, ningependa kusoma na kuelewa zaidi namna ya uchanganyaji wa saruji na udongo, ila picha haionekani vema.

    ReplyDelete
  9. Naomba pia kufahamu upatikanaji pamoja na bei ya mashine hiyo.

    ReplyDelete
  10. Majibu yapitie barua pepe yanguamabyo ni:- wilsonephat@gmail.com

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ningependa na mm kujua bei ya mashine nahitaji moja

      Delete
  11. Nahitaji machine mnauza kwa sh. Ngapi

    ReplyDelete
  12. Nami pia nipo interested na kujua bei ya mashine kwa tofali mojamina pia jinsi ya kuchanganya kupata matokeo mazuriasante.

    ReplyDelete
  13. Hello, professional manufacturer of brick making machine from China,
    have specialized in brick making machine for 20 Years.
    Two Kinds Brick Machine : Concrete And Clay.
    Characteristic: Super Quality And Competitive Price.
    Visit and subscribe its Youtube channel to get everything you want,
    https://www.youtube.com/channel/UCT3OEig0wTHSTGOG_vIg_FA

    ReplyDelete
  14. Halo, mtengenezaji mtaalamu wa mashine ya kutengeneza matofali kutoka China,
    kuwa na utaalam katika mashine ya kutengeneza matofali kwa miaka 20.
    Aina mbili za Mashine ya Matofali: Zege Na Udongo.
    Tabia: Ubora wa hali ya juu na Bei ya Ushindani.
    Tembelea na ujiandikishe kituo chake cha Youtube kupata kila kitu unachotaka,

    https://www.youtube.com/channel/UCT3OEig0wTHSTGOG_vIg_FA

    ReplyDelete