Saturday, 18 July 2015

UJENZI WA MATOFALI YA UDONGO SARUJI YA KUFUNGAMANA

Wakati wa ujenzi wa matofali haya hutumii udongo mwashi (mortar) kuyaunganisha kwa kuwa umbo lake linaruhusu kufungamana na kushikana bila tatizo lolote na ndio maana yanaitwa matofali ya kufungamana (interlocking Bricks) isipokuwa katika mstari wa kwanza kabisa chini unaoungana na msingi (foundation) ni lazima uweke udongo mwashi "mortar" ili kuweza kuunganisha ukuta na msingi ili uwe imara zaidi.

 

 
Ujenzi wa matofali ya kufungamana katika hatua za mwanzo huko Lufwisi Sikonge, Tabora


 
Kuanzia mstari (course) wa pili unaendelea kupanga matofali bila kuweka udongo mwashi lakini ukizingatia taratibu na masharti yote ya ujenzi hadi kwenye linta, kisha unafunga linta yako kama inavyotumika katika ujenzi wa aina nyingine ya matofali, au unaweza kutumia matofali ya chaneli ya linta (lintel channel) katika kufunga linta na kwa kutumia njia hii hautahitaji kufunga box la mbao kwa ajili ya linta isipokuwa matofali yenyewe yanachukua nafasi ya box la mbao hivyo kutohitajika matumizi ya mbao kwa ajili ya kufunga linta.

Linta ya box ilitumika katika ujenzi wa Ofisi ya Mbunge wa Manyoni-Singida

Muonekano wa Ofisi hiyo baada ya kuezekwa
 

Nyumba hizi zimefungwa linta kwa kutumia matofali ya linta chaneli huko Miyuji-DodomaMatofali ya kufungamana pia hutumika katika ujenzi wa uzio (fence) kama picha hapo chini zinavyoonyesha.

 
 
Nyumba hii na uzio wake iko Mikocheni B Dar es salaam


Mwananchi, hujachelewa bado wasiliana na NHBRA kupata huduma zao ili nawe uweze kumiliki nyumba, wasiliana nasi kwa simu namba +255 679 972 715 au dawatilamsaada@nhbra.go.tz

 

No comments:

Post a comment