Friday, 16 June 2017

TAARIFA KWA UMMA

Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) unapenda kuutangazia Umma kwamba katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma 2017, Wakala unawakaribisha wananchi kutoa malalamiko na kero zao kwa kutembelea ofisi ya NHBRA iliyopo Mwenge jijini Dar Es Salaam, kutuma barua pepe (dawatilamsaada@nhbra.go.tz) au kupiga simu kupitia nambari 0679 972 715. Huduma hii itaanza tarehe 16/06/2017-23/06/2017 kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.

No comments:

Post a comment