Tuesday, 17 January 2017

NHBRA YACHANGIA MADAWATI

 
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi umepata nafasi ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha hali ya sekta ya elimu Nchini. Wakala  umetengeneza madawati 50 ambayo yamekabidhiwa Shule ya Msingi Mavurunza iliyopo Kimara katika Manispaa ya Ubungo.
 
Walimu na wanafunzi waliohudhuria katika hafla ya kukabidhi madawati
Walimu wakifuatilia kwa karibu matukio wakati wak ukabidhi madawati shuleni Mavurunza
 Dawati lililotengenezwa na NHBRA
Mwakilishi wa MKurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo, Bw. Hussein Masoud (wa kwanza kulia) akiwakaribisha wageni kutoka NHBRA pamoja na wajumbe wa kamati ya Shule katika hafla ya kukabidhi madawati. kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mavurunza Bw. Robert Mwakimi
Kaimu Meneja wa Biashara na Utawala Bi. Hadija Maloya akikabidhi madawati kwa mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bw. Hussein Masoud
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mavurunza wakiwa wamekalia madawati yaliyokabidhiwa na NHBRA


2 comments:

  1. kazi nzuri imefanywa na wakala; wakala ujishushe Zaidi kwa wananchi wa chini kwani wanamatarajio makubwa sana kutoka kwao. hasahasa katika ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. hongereni sana

    ReplyDelete