Tuesday 7 July 2015

IJUE NHBRA

National Housing and Building Research Agency-NHBRA ni Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi. Ni wakala wa Serikali ambao ulianzishwa mwaka 2001. Wakala huu uko chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ukiwa na jukumu la kufanya utafiti wa vifaa vya ujenzi vipatikanavyo hapa nchini kwa lengo la kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba ili kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora na imara kwa gharama nafuu.

Katika kufanikisha ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu, NHBRA inashauri wananchi watumie teknolojia ya matofali ya kufungamana katika ujenzi wa nyumba zao kwani matofali haya yanatengenezwa kwa kutumia udongo na saruji kidogoili kuwezesha tofali kuwa imara zaidi. Matofali haya yanatengenezwa na mashine maalum ambayo itakuwezesha kutoa umbo la kufungamana kwa matofali ya aina mbalimbali ambayo hutumika katika ujenzi wa nyumba.


                                             Mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana

inaaminika kwamba sehemu kubwa ya nchi yetu udongo unapatikana kwa wingi hivyo wananchi wakiweza kuzipata mashine hizi wataweza kufyatua matofali haya na kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba bora na imara kwa gharama nafuu.

                                     Tofali hizi zimefyatuliwa huko Lukokoda wilayani Tandahimba

Tandahimba ina udongo unaofaa sana katika kutengeneza tofali hizi, wananchi wa Tandahimba jiwezeshe tukuwezeshe kumiliki nyumba bora na imara kwa gharama nafuu kabisa. kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu +255 22 2771971 au info@nhbra.go.tz vile vile unaweza kutoa maoni yako hapa karibuni sana



6 comments:

  1. Habari..mimi ni mjasiriamali mdogo wa kitanzania ambaye nina mashinr kubwa ya tofali za interlocks yenye uwezo wa tofali 2000 kwa siku..je? Nawezaje pata masoko nje ya mkoa wa dar es salaam...

    ReplyDelete
  2. Habari yako Amani Twaha, nina maswali machache kwako.
    1. je mashine yako ni ya kawaida ya mkono au ya kutumia umeme?
    2. je unaweza ukanitumia picha yake kwa email yetu ya nhbra2001@gmail.com?

    ReplyDelete
  3. Njema..mashine yangu ni ya kutumia diesel na ni mobile...ina fyatua tofali 2000 kwa siku..picha nimekutumia

    ReplyDelete
  4. Njema..mashine yangu ni ya kutumia diesel na ni mobile...ina fyatua tofali 2000 kwa siku..picha nimekutumia

    ReplyDelete
  5. Habari ya Asubuhi Amani Twaha, naomba uniandikie namba yako ya simu kwa mawasiliano Zaidi.

    ReplyDelete
  6. namba yangu ya simu ni;0654011152

    ReplyDelete