Tuesday, 18 September 2018

KAIMU MKURUGENZI WA NHBRA ATEMBELEA KARAKANA NA WAKALA

Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Bw. Dismass Minja, alipata nafasi ya kuangalia baadhi ya Tafiti zilizofanywa na Wakala pamoja na Tafiti nyingine zinazoendelea.

Meneja wa Utafiti Eng. Benedict Chilla akitoa maelezo ya Tafiti zinazoendelea juu vigae vya kuchoma, kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wakala Bw. Dismass Minja 


Kaimu Mkurugenzi wa NHBRA akiangalia utengenezaji wa ''Waffles'' ambayo pia ni miongoni mwa Tafiti zilizokamilika. Teknolojia hii mpya kwa Tanzania hutumika zaidi katika ujengaji wa nyumba za ghorofa 

Fundi Sanifu akitoa maelezo juu ya mashine ya kufyatulia matofali ya kufungamana ambayo bado iko kwenye tafiti yenye uwezo wa kutoa matofali mawili.

Meneja Utafiti na Maendeleo akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi juu ya utengenezaji wa kigae mkonge




Kaimu Mkurugenzi akiangalia fremu ya mlango wa zege ambayo tayari imeshawekwa ukutani. Fremu hizo zimeonekana kuwa zitakuwa suluhisho kubwa kwa Watanzania wanaolalamika mchwa kuharibu milango yao
Kaimu Mkurugenzi akiangalia ufyatuaji wa tofali la kufungamana


Kaimu Mkurugenzi akifanya jaribio la kutoa tofali katika mashine ya kufungamana

Kwa mawasiliano zaidi juu ya namna ya kupata mashine ya matofali ya kufungamana, kununua tofali, vigae mkonge na kupata mafunzo usisite kututafuta kwa namba ifuatayo;

0679972715

au

Barua pepe: dawatilamsaada@nhbra.go.tz

au

Fika ofisini kwetu Mwenge tunapakana na kituo cha mafuta cha Oilcom.

Karibuni sana.

Monday, 3 September 2018

JESHI LA MAGEREZA LAVUTIWA NA TEKNOLOJIA YA UJENZI WA GHARAMA NAFUU

Jeshi la Magereza (Tanzania Prison Service) haliko nyuma katika kusambaza teknolojia ya ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu. Baadhi ya Askari wa Jeshi hilo kutoka Lindi na Tanga walifika NHBRA kuanzia tarehe 20/08/2018-02/09/2018 kwa ajili ya kupata mafunzo ya namna ya kutumia mashine ya matofali ya kufungamana na jinsi ya kujenga kwa kutumia tofali hizo ambapo pia waliahidi kusambaza teknolojia hii kwa jamii iliyowazunguka. 

Askari kutoka Jeshi la Magereza wakiwa kwenye jaribio la kufyatua tofali la kufungamana katika ofisi za NHBRA






Washiriki kutoka Jeshi la Magereza wakitoa tofali la kufungamana kutoka kwenye mashine ya matofali ya kufungamana

Askari wa Jeshi la Magereza wakifanya setting ya nyumba katika mafunzo ya ujenzi wa nyumba kwa kutumia matofali ya kufungamana yanayotolewa na NHBRA







Ili kuweza kupata mafunzo kama haya, mteja unashauriwa kununua mashine ya matofali ya kufungamana kwa gharama ya shilingi 650,000/- ambapo malipo hayo mteja atapaswa kulipia benki. Na baada ya kununua mashine Mteja atapata mafunzo kwa vitendo juu ya utumiaji wa mashine ya tofali za kufungamana pamoja na namna ya kujenga kwa muda wa wiki moja kulingana na uelewa wa vijana ambao Mteja atakuwa amewaleta wasiozidi watatu.

Kwa mawasiliano zaidi, usisite kututafuta kwa namba ifuatayo;

0679972715

au

Barua pepe: dawatilamsaada@nhbra.go.tz

au

Fika ofisini kwetu Mwenge tunapakana na kituo cha mafuta cha Oilcom.

Karibuni sana.

Wednesday, 1 August 2018

TEKNOLOJIA YA NHBRA YAZIDI KUJULIKANA

Washiriki wa semina ya ''Adequate Housing'' kutoka Uganda, Kenya, Mozambique, Zambia na wenyeji wao Tanzania walipata nafasi ya kutembelea Wakala wa Taifa wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi ili kuweza kujionea shughuli mbalimbali za Wakala.








                           












Monday, 30 July 2018

WAFANYAKAZI WA NHBRA WAONGEZEWA UWEZO

NHBRA ilipata nafasi ya kuhudhuria semina ya Uhamasishaji kwa watumishi ili kusaidia katika kuongeza ufanisi katika majukumu ya kila siku wawapo kazini. Mada mbalimbali zilitolewa mfano namna ya Utendaji kazi Serikalini, maadili katika Utumishi wa Umma n.k. Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa UDBS-UDSM.
Semina hiyo ilihudhuriwa na watoa mada kutoka Utumishi ya Umma pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

HABARI PICHA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHBRA akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye semina ya uhamasishaji kwa watumishi wa Wakala kwenye ukumbi wa UDBS-UDSM


Kaimu Meneja wa Biashara na Utawala wa NHBRA Bi. Hadija Maloya akitoa ufafanuzi juu ya huduma zitolewazo katika kitengo cha Biashara




Tuesday, 3 July 2018

TUPO SABASABA

Tunautangazia Umma kwamba Nhbra Tanzania inashiriki Maonyesho ya 42 ya Kitaifa ya Biashara-Sabasaba. Tembelea Banda letu lililopo katika hema la Katavi Banda namba 11-13 ili upate kufahamu na kujionea tafiti zetu kama mashine za matofali ya kufungamana, nyumba ndogo ya mfano iliyojengwa kwa tofali za kufungamana na kuezekwa kwa kutumia vigae vya gharama nafuu, pamoja na teknolojia yetu mpya ya fremu za milango za zege pamoja na sakafu ya dari "waffles"... KARIBUNI SANAAAAAAA tuko hapa mpaka tarehe 13/7/2018.

Moja wapo ya teknolojia mpya za ujenzi tulizoenda nazo sabasaba ni ujenzi kwa kutumia ''waffles'' kama ilivyo kwenye picha upande wa kushoto ni mwonekano wa waffles ikiwa tayari imejengwa kwa mfano wa ujenzi wa nyumba ya ghorofa. karibuni sabasaba mje mpate maelezo ya kina juu ya teknolojia hii.

Mwonekano wa banda letu sabasaba

Baadhi ya washiriki kutoka NHBRA wakiwa tayari kutoa maelezo ya kina kuhusu teknolojia ya gharama nafuu

Mgeni aliyetutembelea akipata maelezo kuhusu teknolojia yetu mpya ya kujenga nyumba ya ghorofa kwa kutumia ''waffles''

Mgeni alietutembelea akiangalia kwa umakini teknolojia yetu mpya ya ujenzi wa nyumba ya ghorofa kwa kutumia waffles


Wananchi wakipata maelezo juu ya utengenezaji wa tofali za kufungamana
Karibuni sanaaaaa......