Monday 30 September 2019

JESHI LA MAGEREZA LAENDELEA KUELIMIKA NA TEKNOLOJIA YA NHBRA

NHBRA, ilipata nafasi ya kutoa Semina ya ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu kwa kutumia vifaa vilivyotafitiwa na Wakala. Semina hiyo ilikuwa ni miongoni mwa mada katika utoaji wa Mafunzo ya Uongozi daraja la juu No.23/2019 kwa Maafisa Magereza, Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania kilichopo Ukonga Dar es Salaam.

Mhandisi Twwimanye John kutoka NHBRA akiwasilisha mada ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa Maafisa Magereza
Afisa wa Magereza akiuliza swali kwa Mhandisi ili kupata ufafanuzi zaidi


Fundi Sanifu Mwandamizi Sylvester Shumbusho akitoa elimu kwa vitendo ya namna ya kutengeneza kigae kwa kutumia mashine mtetemo

Maafisa Magereza wakifanya jaribio la kutengeneza kigae mkonge 
Maafisa wa Magereza wakiwakilisha baadhi ya Wanawake katika Semina hiyo nao hawakua nyuma kufanya majaribio hayo ya utengenezaji wa kigae mkonge

Maafisa Magereza wakifuatilia kwa umakini utengenezaji wa tofali la kufungamana kwa kutumia mashine iliyotafitiwa na NHBRAKwa mawasiliano zaidi juu ya namna ya kupata mashine ya matofali ya kufungamana, kununua tofali, vigae mkonge na kupata mafunzo usisite kututafuta kwa namba ifuatayo;

+255 679 972 715

au

Barua pepe: dawatilamsaada@nhbra.go.tz

au

Fika ofisini kwetu Mwenge tunapakana na kituo cha mafuta cha Oilcom.

Karibuni sana

BEI MPYA YA BIDHAA ZA KARAKANA