Friday 20 January 2017

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA NHBRA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii leo tarehe 20 Januari, 2017 imetembelea Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa kazi na changamoto zinazoikabili Wakala. Yafuatayo ni baadhi ya matukio katika picha yakionyesha ziara ya Kamati hiyo.

Mh. Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Angeline Mabula akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala Dkt. Matiko Mturi mara baada ya kuwasili Ofisini za NHBRA.

Mh. Naibu Waziri Bi. Angeline Mabula akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili NHBRA

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Naibu Waziri pamoja na Meneja wa Biashara na Utawala, Bi. Hadija Maloya (wakwanza kulia) wakiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.


Kamati ya Bunge wakikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara na Wakala

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge

Afisa Biashara, Bi. Zubeda Salum akitoa maelezo kuhusu Wakala kwa Kamati ya  Bunge pamoja na wawakilishi wa Wizara

Mkurugenzi Mkuu akielezea kuhusu moja ya chapisho za tafiti zilizofanywa na Wakala

Fundi Sanifu, Bw. Hussein Mataka akitoa ufafanuzi juu ya uezekeaji wa nyumba kwa kutumia vigae vinavyotengenezwa na Wakala





Fundi Sanifu Bw. Sylvester Shumbusho akielezea namna ya kutengeneza kigae cha kuchoma kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge

 
Naibu Waziri akifuatilia maelezo ya namna ya kutengeneza vigae vya kuchoma 

Mhandisi Amri Juma akitoa maelekezo ya ujenzi wa matofali ya kufungamana yanayotengenezwa kwa udongo tu bila saruji

Mkurugenzi Mkuu akitoa maelezo juu ya vigae vinavyotengenezwa na Wakala

Kamati ya Kudumu ya Bunge ikiangalia vigae hivyo vilivyokuwa tayari kwa kuezekewa

Mkurugenzi Mkuu akielezea kuhusu uchanaganyaji wa nyuzi za katani katika utengenezaji wa vigae vya kuezekea nyumba


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge pamoja na wafanyakazi wa Wakala wakifurahia jambo kwa pamoja

Naibu Waziri akielezea jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge

Mkurugenzi Mkuu akiagana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo mara baada ya kumaliza ziara yao
 

Tuesday 17 January 2017

NHBRA YACHANGIA MADAWATI

 
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi umepata nafasi ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha hali ya sekta ya elimu Nchini. Wakala  umetengeneza madawati 50 ambayo yamekabidhiwa Shule ya Msingi Mavurunza iliyopo Kimara katika Manispaa ya Ubungo.
 
Walimu na wanafunzi waliohudhuria katika hafla ya kukabidhi madawati
Walimu wakifuatilia kwa karibu matukio wakati wak ukabidhi madawati shuleni Mavurunza
 Dawati lililotengenezwa na NHBRA
Mwakilishi wa MKurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo, Bw. Hussein Masoud (wa kwanza kulia) akiwakaribisha wageni kutoka NHBRA pamoja na wajumbe wa kamati ya Shule katika hafla ya kukabidhi madawati. kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mavurunza Bw. Robert Mwakimi
Kaimu Meneja wa Biashara na Utawala Bi. Hadija Maloya akikabidhi madawati kwa mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bw. Hussein Masoud
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mavurunza wakiwa wamekalia madawati yaliyokabidhiwa na NHBRA


Thursday 5 January 2017

NAMBA YA SIMU YA HUDUMA KWA WATEJA

NHBRA sasa imeweka namba rasmi ambayo mteja anaweza kupiga na kusikilizwa...
Kwa maswali na ushauri piga namba hii +255 679 972 715
Muda ni kuanzia saa moja na nusu asubuhi mpaka saa tisa na nusu mchana.
KARIBUNI