Monday, 1 October 2018

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAKAZI DUNIANI

Maadhimisho ya Siku ya makazi Duniani kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya ''UDHIBITI WA TAKA NGUMU MIJINI'' kongamano la maadhimisho hayo linafanyika Mkoani Dodoma kwenye Ukumbi wa Hazina (Treasury Square).
NHBRA kama mdau katika kufanya Tafiti za vifaa bora vya ujenzi na vyenye gharama nafuu inawatakia heri katika kuadhimisha siku ya Makazi Duniani 2018. Pia inawashauri wananchi kuendelea kutumia teknolojia za ujenzi wa nyumba zilizotafitiwa na Wakala huu kwa kuwa ni rafiki kwa utunzaji mazingira. Aidha inahamasisha wananchi kuendelea kudhibiti uzalishaji wa taka ngumu pamoja na kutumia teknolojia mbadala za kubadilisha taka ngumu kuwa vifaa mbalimbali vitakavyotumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo ya ujenzi wa nyumba mijini na vijijini.


No comments:

Post a Comment