Wednesday, 2 May 2018

MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI

Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani hufanyika kila mwaka tarehe moja ya mwezi wa tano (mei mosi). Mwaka huu kwa Taifa la Tanzania maadhimisho hayo yalifanyika katika Mkoa wa Iringa ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.

Mkoa wa Dar es Salaam nao haukua nyuma katika kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa Wafanyakazi, ambayo ilifanyika katika uwanja wa Taifa. NHBRA ilipata nafasi ya kuhudhuria maadhimisho hayo ikiwa na kauli mbiu ya ''maendeleo ya viwanda yawe chachu katika kuongeza tafiti za ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu''.

Wafanyakazi wa NHBRA wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani



No comments:

Post a Comment