Mwendelezo wa toleo lililopita.............
Ujenzi wa nyumba
umegawanyika katika hatua zifuatazo: -
•
Kupima msingi wa
jengo
•
Kuchimba msingi
•
Kumwaga zege la
msingi
• Kujenga kuta za msingi
•
Kuweka kifusi na
kushindilia
•
Kupanga mawe
•
Kumwaga zege la jamvi
•
Kujenga kuta za boma
• Kumwaga zege la linta
•
Kujenga juu ya linta
•
Kupaua jengo
•
Kuweka milango na
madirisha
•
Kazi za umaliziaji na
kazi za huduma mbalimbali mfano; umeme, maji, simu n.k
• Ni muhimu kupata
ushauri wa kitaalamu wakati wa utengenezaji wa tofali za msingi kuhusu
uchanganyaji wa udongo na saruji. Vipimo vya unene vya ukuta wa msingi na kina
hutegemea na aina ya jengo na sifa za udongo uliopo, inashauriwa kina kisiwe
chini ya sentimeta 45 na unene wa ukuta wa msingi usiwe chini ya sentimeta 30
(urefu wa tofali moja).
Kuseti kuta za boma
• Hatua inayofuata ni kuseti kuta za boma kwa kutumia
ramani iliyopo. Hatua hii hufanyika kwa namna mbili: kwanza ni kuyapanga
matofali kwa kuzingatia vipimo vya urefu wa kuta na kuondoa tofali maeneo yote
ya uwazi kama milango na maeneo ya wazi ambayo yana mwendelezo wa ujenzi baada ya
linta. Vipande robo tatu tofali hutumika wakati wa kugawa vyumba na kwenye
maungio msalaba
Kujenga kuta za boma
• Tofali huunganishwa
kwa udongo mwashi kwenye kitako (bed jointing). Ni muhimu kutumia udongo mwashi
kwenye kozi ya kwanza ili kuweka muunganiko kati ya sehemu ya chini ya
nyumba(substructure) na ile ya juu (superstructure). Katika hatua hii ni lazima
kuhakikisha kuwa kuta zinanyooka na zina pimamaji. Ikumbukwe kuwa kuanzia kozi ya 2 hadi kwenye ring beam tofali hujengwa
bila kutumia udongo saruji. Hata hivyo, kwa ajili ya kuongeza uimara udongo saruji
laini (1:3) huwekwa kwenye kona, kwenye makato ya milango na madirisha. Kozi ya 2, kwa kuta za kugawa vyumba unaanza
na tofali mbili za robo tatu ili kuondoa mfuatano wa maungio wima(straight
vertical joints).
• Vipande
vya nusu tofali hutumika zaidi kwenye makato ya madirisha na milango ili
kuondoa mfuatano wa maungio wima.
Kutengeneza na kufunga boksi
• Utengenezaji wa box
hufanyika kwa kuunganisha kwanza mbao za pembeni, kwa kutumia vibao maalum na
kisha kulipachika ukutani na kuunganishwa na mbao za sahani kwa kutumia
misumari. Box ni lazima liimarishwe vizuri pamoja na kuweka mirunda sehemu zote
stahiki ili kuzuia kupinda au kuyumba kwa box hilo wakati wa kuweka zege.
Ujenzi wa matofali mfereji (channel blocks)
• Hii ni teknolojia
ambayo hupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya mbao/miti kama vifaa vya
kutengeneza kalibu ya kushika zege laini, ambapo matofali yenye umbo la kalibu
hujengwa juu ya mstari wa mwisho kabla ya linta kwa lengo la kupokea zege
laini. Kwa kuwa matofali hayo hufanana na tofali nyingine huficha eneo lenye
linta na kufanya nyumba ionekane vizuri (Disappearing formwork).
• Hapa matumizi ya mbao
za sahani na mirunda ni kwenye madirisha, milango na maeneo mengine yaliyo
wazi, ambapo kuna linta. Njia hii ni bora, rahisi na rafiki kwa mazingira kwani
hupunguza matumizi ya miti/mbao.
Kumwaga zege la linta
• Kabla ya kumwaga zege
ni bora kufanya yafuatayo kwanza; kuweka nondo, kuweka nyaya za kufungia wall
plates na kuweka mabomba ya umeme (conduit pipe) kwa nyumba yenye huduma ya
umeme. Pia vipande vya mbao vyaweza kutumika kuweka matundu kwenye zege na
kuvitoa zege likishanyauka kwa ajili ya kupitisha bomba za umeme pale ambapo
kazi ya umeme itafanyika baadae na si lazima kununua bomba kipindi hicho kazi
ya kumwaga zege ni kama inavyofanyika kwenye ujenzi wa kawaida isipokuwa tu, ni
lazima kuhakiki kuwa mabomba ya umeme yako wima.
Ujenzi wa tofali juu ya linta
• Kozi ya kwanza baada ya linta, udongo mwashi hutumika
ili kuunganisha linta na ukuta wa juu. Pia kulingana na ramani ukuta wa hanamu
(gable) hujengwa baada ya kukamilika kwa hizo kozi 4. Ni muhimu matundu ya
tofali kwa kuta zilizopo juu ya linta yajazwe udongo saruji laini.
impresive
ReplyDeleteipo vyema
ReplyDelete