Monday, 25 April 2016

NHBRA YAPATA MKURUGENZI MKUU


Hatimae NHBRA imepata Mkurugenzi Mkuu, Dr. Matiko Samson Mturi ambae ameripoti tangu mwezi Februari, 2016. Wafanyakazi wote kwa pamoja wanakukaribisha sana NHBRA. kwa pamoja tutaweza na kuyafikia malengo yaliyowekwa. Karibu sana Dr Mturi.

Sunday, 17 April 2016

VIJUE VIFAA VYA UJENZI

Vifaa vya ujenzi vinaweza kupatikana kutokana na chanzo cha ardhi au mimea. vifaa vinavyotokana na ardhi ni kama vile mawe na miamba, madini mbalimbali na udongo ambao unapatikana kama kokoto, mchanga, tifutifu (SiH) na mfinyanzi. Kwa upande wa madini ni kama vile chokaa, chuma, aluminium na gypsum. Vifaa vinavyotokana na mimea ni kama vile magogo, mbao, fito, boriti, kamba na makuti.

Sifa za vifaa bora vya ujenzi ni kama ifuatavyo:

  1. Vifaa imara na vyenye ubora
  2. Vinavyodumu na kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa
  3. Viweze kufanyiwa kazi na kuwekwa kwenye vipimo
  4. Vipatikane kirahisi
  5. Vinavyovutia na kukubali nakshi
  6. Vinavyopatikana kwa urahisi
  7. Vyenye gharama nafuu
  8. Visivyoharibu mazingira

Nyumba zilizojengwa kwa ukuta wa matofali ya udongo saruji na mabanzi

Sehemu kuu za nyumba
  1. Msingi
  2. Sakafu
  3. Ukuta
  4. Dari (Pauo-roof structure)
  5. Paa (Ezeko-roof covering)

Vifaa vya kujenga Msingi

  1. Mawe
  2. Matofali ya kuchoma
  3. Matofali ya udongo yaliyoimarishwa kwa saruji/chokaa
  4. Matofali ya zege (mchanganyiko wa kokoto, mchanga na saruji)
  5. Udongo mwashi
  6. Zege
  7. Miti 

Vifaa vya kujenga sakafu

  1. Mawe
  2. Kifusi kilichoshindiliwa
  3. Udongo ulioimarishwa kwa saruji au chokaa
  4. Zege
  5. Matofali ya kuchoma
  6. Mbao

Vifaa vya kujenga ukuta

  1. Matofali ya udongo mtupu/saruji/chokaa au mchanga na saruji
  2. Udongo mtupu
  3. Zege
  4. Chuma
  5. Mianzi
  6. Mabanzi
  7. Fito
  8. Kamba zinazotokana na mimea

Vifaa vya kujenga dari

  1. Mbao
  2. Udongo
  3. Zege
  4. Miti
  5. Mkeka wa mianzi
  6. Chipboard/hardboard/gypsum

Vifaa vya kujenga paa

  1. Boriti
  2. Mabati
  3. Vigae
  4. Zege
  5. Makuti
  6. Misumari
  7. Kamba
Tumia vifaa imara na madhubuti ili upte nyumba bora, imara na ya kudumu. pamoja na vifaa hivyo, vile vile ni vizuri kutumia teknolojia madhubuti na sahihi katika ujenzi wa nyumba yako. kwa ushauri zaidi watembelee NHBRA au wasiliana nao kwa kutumia simu +255 22 2771971 au barua pepe info@nhbra.go.tz




 


 


 

TAARIFA KWA WADAU WETU WOTE

Wapendwa mashabiki na wadau wa blog hii, tunaomba radhi kwa kutoruisha habari kwa muda mrefu, hali hiyo ilitokana na matatizo ambayo yalikuwa juu ya uwezo wetu. sasa tumerudi tutaendelea kuelimishana kuhusu masuala ya utafiti na ujenzi wa gharama nafuu kwa kutumia teknolojia rahisi kabisa ya ujenzi wa nyumba. Nyote mnakaribishwa.